1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump ataka jumuiya ya NATO imkabidhi Greenland

21 Januari 2026

Hotuba ya rais wa Marekani mbele ya kongamano la kiuchumi duniani mjini Davos imewakosoa viongozi wa Ulaya na kuiita jumuiya ya NATO kuwa dhaifu isiyokuwa na uwezo wa kutowa ulinzi kwa Greenland

https://p.dw.com/p/57CAw
Rais Trump amedai kwenye kongamano la Davos kwamba  muungano wa NATO haujawahi kuwa na faida kwa Marekani
Rais Trump amedai kwenye kongamano la Davos kwamba muungano wa NATO haujawahi kuwa na faida kwa MarekaniPicha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images

Rais Donald Trump ameinadi nchi yake kwamba ndio pekee yenye uwezo duniani wa kuihakikishia usalama Greenland, akidai hakuna mshirika yoyote wa Jumuiya ya Nato anayeweza kukilinda kisiwa hicho cha barafu isipokuwa Marekani:

''Nawaheshimu sana watu wa Greenland na watu wa Denmark. Lakini kila mshirika wa NATO ana wajibu wa kuwa na uwezo wa kujilinda lakini ukweli ni kwamba hakuna nchi moja  wala kundi la  nchi zilizokuwa kwenye nafasi ya kuweza kuilinda Greenland isipokuwa Marekani.Ni nchi yenye nguvu na tuna nguvu kuliko watu wanavyoelewa.''

Utawala wa Trump watishia kuvunjika kwa uhusiano wa Atlantiki

Akizungumza mbele ya Jukwaa la kiuchumi duniani Trump ameitisha mkutano wa haraka kuhusu azma hiyo ya Marekani ya kukitwaa kisiwa hicho chenye kujitawala ambacho ni sehemu ya Denmark, nchi mwanachama wa Jumuiya ya mfungamano wa kijeshi wa NATO ambao ameukosowa akisema hauna faida yoyote kwa Marekani. Greenland

Rais huyo wa Marekani ambaye anakosolewa na viongozi wa Ulaya amewashambulia akisema Ulaya haina mwelekeo mzuri.