1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump ampokea Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman

19 Novemba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amempokea katika Ikulu ya White House Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman na wakasaini mikataba ya kibiashara na kiulinzi.

https://p.dw.com/p/53r8p
Washington I Trump akiwa na mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman
Rais wa Marekani Donald Trump akiwa na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Utawala wa Trump umesema Saudi Arabia itaongeza mipango yao ya uwekezaji kutoka dola bilioni 600 hadi takriban dola trilioni 1. Riyadh imekubali pia kununua ndege za kivita na vifaru karibu 300 vya Marekani.

Akihojiwa na waandishi wa habari,  Trump alimtetea Bin Salman  na kusema Mwanamfalme huyo hakuwa na taarifa zozote kuhusu mauaji ya mwaka 2018 ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi aliyeuawa ndani ya Ubalozi wa Saudia mjini Istanbul.