SiasaAsia
Taiwan yasema ni taifa "huru" baada ya onyo la Trump
16 Mei 2026
Matangazo
Taiwan imesema ni taifa huru na la kidemokrasia, saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kukionya kisiwa hicho dhidi ya kutangaza rasmi uhuru wake kutoka China. Kauli hiyo imekuja baada ya Trump kumaliza ziara nchini China, ambapo Rais Xi Jinping alimhimiza kutoiunga mkono Taiwan.
Wizara ya mambo ya nje ya Taiwan imesema taifa hilo haliko chini ya Jamhuri ya Watu wa China na kwamba mauzo ya silaha kutoka Marekani ni sehemu ya makubaliano ya usalama kati ya pande hizo mbili.
Trump amesema hataki kuona vita vikizuka kuhusu Taiwan na amezitaka Taiwan na China "kupunguza mvutano". China inaiona Taiwan kama sehemu ya eneo lake na imekuwa ikiongeza shinikizo la kijeshi katika miaka ya karibuni.