1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stoltenberg asema Sweden imeonesha kushindwa kwa Putin

11 Machi 2024

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, amesema kujiunga kwa Sweden katika muungano huo wa kijeshi kunaonesha kushindwa kwa Rais Vladmir Putin kwenye mkakati wa kuidhoofisha jumuiya hiyo kupitia vita vya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4dOe9
Sweden yajiunga rasmi na NATO
Waziri Mkuu wa Sweden, Ulf Kristersson, (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya NATO, Jens Stoltenberg, kwenye makao makuu ya jumuiya hiyo mjini Brussels, Ubelgiji, siku ya Jumatatu (11 Machi 2024).Picha: Kenzo Tribouillard/AFP

Stoltenberg alisema siku ya Jumatatu (Machi 11) kwamba sio tu uvamizi wa Urusi uliyachochea matatifa yaliyokuwa hayafungamani na upande wowote, yaani Sweden na Finland, kuwa chini ya mwamvuli wa ulinzi wa NATO, lakini pia sasa Ukraine iko karibu zaidi kuwa mwanachama wa muungano huo wa kijeshi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Soma zaidi: Sweden yajiunga na NATO na kuwa mwanachama wa 32

Katika kujibu vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, NATO imeongeza uwepo wetu kote katika eneo hilo, na uwanachama wa Sweden unazidi kudhihirisha hilo." Alisema Katibu Mkuu huyo wa NATO.

"Wakati Rais Putin alipoanzisha uvamizi wake kamili miaka miwili iliyopita, alitaka NATO idhoofike na awe na udhibiti zaidi dhidi ya majirani zake. Alitaka kuiharibu Ukraine kama taifa huru, lakini akashindwa." Aliongeza. 

Soma zaidi: NATO iliyotanuliwa yaanza luteka Finland, Norway na Sweden

Stoltenberg aliyasema hayo akiwa na Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson, muda mfupi tu kabla ya bendera ya Sweden kupandishwa katika makao makuu ya NATO mjini Brussels katika hafla ya kuikaribisha rasmi Sweden kuwa nchi mwanachama wa 32 wa muungano huo.