Migogoro
NATO iliyotanuliwa yaanza luteka Finland, Norway na Sweden
4 Machi 2024Matangazo
Zaidi ya wanajeshi 20,000 kutoka mataifa 13 wanashiriki katika mazoezi hayo yatakayochukua karibu wiki mbili kwenye maeneo ya kaskazini ya Finland, Norway na Sweden.
Wizara ya ulinzi ya Finland, ambayo ni mwanachama mpya wa NATO, imesema wanajeshi wake zaidi ya 4,000 wanashiriki kwa mara ya kwanza katika operesheni ya ulinzi wa pamoja wa kikanda kwenye muungano huo.
Soma pia: Mazoezi makubwa ya kijeshi ya NATO yaanza Norway
Finland iliyo na mpaka wa kilomita 1,340 kati yake na Urusi, ilijiunga na NATO mnamo mwezi uliopita. Nchi jirani yake ya Sweden kwa sasa imo kwenye mchakato wa kukamilisha taratibu za kuingia katika muungano wa kijeshi wa NATO kama mwanachama wake wa 32.