Siku ya wafanyakazi duniani. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 01.05.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Siku ya wafanyakazi duniani.

Watu zaidi na nusu milioni washiriki katika mikutano ya hadhara kuadhimisha Mei Mosi nchini Ujerumani.

Mwenyekiti wa jumuiya kuu ya wafanyakazi Ujerumani Michael Sommer.

Mwenyekiti wa jumuiya kuu ya wafanyakazi Ujerumani Michael Sommer.

Mikutano ya hadhara inafanyika katika miji mikubwa kadhaa ya Ujerumani kuadhimisha siku ya wafanya kazi duniani.

Na kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano mwenyekiti wa chama cha Social Demokratik , kilichomo katika serikali ya mseto ya Ujerumani ameshiriki katika maadhimisho hayo.

Mikutano hiyo ya hadhara inafanyika katika miji mikubwa maaruf ya Nürneberg,Hamburg na Berlin.

Maandamano ya wafanyakazi pia yanafanyika katika mji mkuu wa jimbo la Rheinland Palatinate kusini magharibi mwa Ujerumani ambapo mwenyekiti wa chama cha Social Demokratik SPD ameshiriki, kwa mara ya kwanza baada ya kujiweka kando na harakati za tabaka la wafanyakazi kwa zaidi ya miaka mitano.

Mwenyeki huyo bwana Kurt Beck amewahutubia wafanyakazi katika kilele cha maadhimisho kwenye mji wa Mainz, katika wadhifa wake kama waziri mkuu wa jimbo la Rheinland Palatinate.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa jumuiya kuu ya wafanyakazi nchini Ujerumani DGB bwana Michael Sommer ameilaumu serikali ya Ujerumani kwa kusababisha kuenea kazi za ujira wa ngama nchini kote. Bwana Sommer amesema mamilioni ya wafanyakazi nchini Ujerumani wanalipwa mishahara ya kuponea, hali inayosababisha umasikini.

Mwenyekiti huyo wa jumuiya kuu ya wafanyakazi ya Ujerumani ameeleza kuwa idadi ya wafanyakazi wanaolipwa mishahara ya kawaida inazidi kupungua nchini.

Kutokana hayo dadi ya masikini inaongezeka na kuwa kubwa wakati watu wachache tu wanazidi kuwa tajiri. Ametilia maanani kuwaa watu zaidi ya milioni moja wanapata malipo ya chini kiasi kwamba wanalazimika kupata msaada kutoka kwenye mfuko wa posho ya kijamii ili kuweza kumudu maisha.

Maadhimisho ya Mei mosi mwaka huu nchini Ujerumani yanafanyika chini ya kaulimbiu inayosema "Lazima pawepo kazi nzuri" na kutokana na hayo, katika mwito wake jumuiya ya wafanyakazi ya Ujerumani inaitaka serikali ya Ujerumani ianzishe utaratibu wa kulipa mshahara wa kima chini katika sekta zote za ajira nchini.

Chama cha wafanyakazi kinataka malipo ya Euro 7 na senti 50 kwa sasa.

Serikali ya Ujerumani pia imetakiwa ichukue hatua ya kukabiliana na kinachofahamika kuwa umasikini miongoni mwa baadhi ya wastaafu.


Akizungumza kwenye maadhimisho hayo mjini Mainz mwenyekiti wa chama cha Social Demokratik, bwana Kurt Beck ambae pia ni waziri mkuu wa jimbo la Rheiland Palatinate pia amesisitiza juu ya utaratibu wa kuanzishwa mshahara wa kima chini katika sekta zote za ajira.

Watu zaidi ya laki tano wameshiriki katika maadhimisho ya Mei mosi nchini Ujerumaani kote.

Hatahivyo sherehe hizo zilikuwa katika tishio la kutiwa dosari na maandamano ya wafuasi wa itikidadi kali za mlengo wa kulia wa chama cha NDP. Chama hicho kimetoa mwito kwa wanachama wake wa kufanya maandamno nchini kote alasiri ya leo.

 • Tarehe 01.05.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Drlj
 • Tarehe 01.05.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Drlj
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com