Siku ya makazi duniani | Masuala ya Jamii | DW | 06.10.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Siku ya makazi duniani

Sherehe za mwaka huu Luanda Angola

Watoto wakichota maji kutoka mtaro wenye maji machafu karibu na Luanda Angola

Watoto wakichota maji kutoka mtaro wenye maji machafu karibu na Luanda Angola

Leo jumatatu ni siku ya makazi duniani.Na inasemekana kuwa zaidi ya watu billion 1.6 duniani hawana mahali pa kulala, na wengine millioni 10 hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayoweza kutibiwa.Kutokana na hali hiyo Umoja wa Mataifa unatoa mwito kwa wahusika kuchukua juhudi za pamoja ili kuoko ulimwengu hasa ukiwapatia makazi wanadamu.

Siku ya makazi duniani ilitengwa kando na Umoja wa Mataifa kufanyika kila mwaka katika siku ya jumatatu ya kwanza ya kila mwezi wa Oktoba.Sherehe za mwaka huu zimefanyika Luanda ,mji mkuu wa Angola,mji ambao ulichaguliwa na shirika hilo kuongoza sherehe za mwaka huu.

Kauli mbiu ya sherehe za mwaka huu ni miji inayoridhisha.Msemaji wa shirika hilo Gert Ludeking amebaini umuhimu wa mji wa Luanda sambamba na sherehe za mwaka huu,akisema kuwa sherehe za Angola zinaonyesha dunia jinsi taifa ambalo limekuwa na migogoro kwa miaka mingi jinsi linavyoendelea kujaribu kuboresha miundo mbinu.

Taarifa zilizopo zinaonyesha kama miji inazidi kupanuka haraka sana ambapo karibu nusu ya walimwengu wwanaishi mijini kuliko mashambani.Msemaji wa shirika la makazi la Umoja wa Mataifa kwanini ulichagua kauli mbiu kutokan na hali ilivyo sasa.Amesema kuwa kauli mbiu hiyo ilichaguliwa ili kutaka kutanabaisha ulimwengu kuhusu athari za ukuaji wa haraka wa miji kuelekea mazingira na vile vile athari kwa maeneo ya miji yenye wakaazi wengi wa kipato cha chini.

Lengo la siku hii,maafisa wa shirika hilo wanasema, ni kutathmini hali ya miji midogo na mikubwa,pamoja na hali za kimsingi za kupata makazi kwa wote.Vilevile lengo lingine ni kuukumbusha ulimwengu kuhusu kuwajibika kwao kueleka mustakbala wa makazi ya mwanadamu.

Bw Gert Ludeking anasema kuwa miji inayoridhisha ni ile inayojumuisha wote ambapo kila mmoja na kila utamaduni unajihisi uko nyumbani.

Watu zaidi billlioni 1.6 duniani hawana makazi na maisha yao ya usoni yako mashakkani.Bila maji safi, wala makazi na matattizo mengine watu wengine millioni 10 hufa kila siku kutokana na magonjwa ambayoweza kutibiwa.Tena watu billioni 1 wanaishi katika maeneo ya madongo poromoka.Ifikapo mwaka wa 2030 inakadiriwa kuwa theluthi mbili ya idadi ya watu duniani itakuwa ya wale wanaishi mijini ikiwa hatua muafka hazitachukuliwa.

 • Tarehe 06.10.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FV2z
 • Tarehe 06.10.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FV2z
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com