Siku ya maji duniani | Masuala ya Jamii | DW | 22.03.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Siku ya maji duniani

Watu zaidi ya bilioni moja duniani wanakosa maji safi ya kunywa

UN wa Mataifa umeeka lengo la kila mwanadamu kupata maji safi ya kunywa kufikia mwaka 2015.Je lengo hilo litafikiwa?

UN wa Mataifa umeeka lengo la kila mwanadamu kupata maji safi ya kunywa kufikia mwaka 2015.Je lengo hilo litafikiwa?

Sehemu kubwa ya ardhi ya dunia imezungukwa na maji.Kwa hali hiyo inaweza kuonekana kwamba kuna kiasi cha kutosha cha maji katika dunia.Asilimia 97,5 ni maji ya bahari na mito pamoja na maziwa.Kiwango kilichosalia cha asilimia 2,5 ni maji maji safi.Takriban theluthi moja ya watu wote duniani hawana maji safi ya kunywa.Na idadi nyingine inagawanya kiasi cha maji kilichosalia.

Hii leo karibu watu billioni 1,1 duniani hawana maji safi ya kunywa na wengine wapatao billioni 2,6 ambao ni kiasi cha thuluthi moja ya watu wa dunia nzima hawapati maji ya kutosha kukidhi huduma zao za siku kwa jumla.Katika malengo ya Millenium ya Umoja wa mataifa imezungumzwa kwamba, maji ni mojawapo ya bidhaa muhimu inayotakiwa kuwafikia watu wote wa dunia kufikia mwaka 2015.

Data za shirika la maji nchini Ujerumani za mwaka 2008 zinaonyesha kwamba matumizi ya maji kwa siku yalifikia lita 122.Nchini Italia kiwango hicho ni lita 800 kwa kila mtu.Kwa mantiki hiyo imeonyesha kwamba matumizi jumla ya maji yanazidi kuongezeka kila uchao.Maji yanatumika sio tu kwa matumizi ya kila siku ya majumbani bali hata kwenye mashamba kwa mfano ya mchele kahawa au pamba.

BdT Indischer Farmer am Welt Wasser Tag

Ukame unatokana na ukosefu wa mvua na kusababisha pia ukosefu wa maji duniani.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la linaloshughulikia mazingira la World wide Fund for Nature WWF unaonyesha kwamba kila mkaazi nchini Ujerumani anahitaji kiwango cha zaidi ya lita 5000 kwa matumizi yake jumla kwa siku.Ingawaje maji ni bidhaa muhimu katika maisha ya mwanadamu lakini bado imesalia kuwa bidhaa ghali kabisa na ambayo haipatikani kiurahisi na kila mtu na pia ubora wake unatofautiana.Matatizo hayo ya maji sio tu yanashuhudiwa katika ulimwengu wa tatu bali ni tatizo la ulimwengu mzima kwa jumla.

Kuna maeneo machache duniani ambayo yana matatizo sugu ya ukosefu wa maji nayo ni pamoja na eneo la Sahel mashariki ya kati na baadhi ya maeneo ya Asia.Nchi nyingi zinazoendelea hilo ni tatizo la kila siku.

Mwandishi Scheschkwewitz Daniel ZR/Saumu Mwasimba

Mhariri AbdulRahman,Mohammed

 • Tarehe 22.03.2010
 • Mwandishi Saumu Ramadhani Yusuf
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MZ1l
 • Tarehe 22.03.2010
 • Mwandishi Saumu Ramadhani Yusuf
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MZ1l
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com