Siku ya kuzaliwa Baba Mtakatifu | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 16.04.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Siku ya kuzaliwa Baba Mtakatifu

Ikiwa ni tarehe 16 Aprili, leo hii ni siku ya kuzaliwa Baba Mtakatifu Benedikt 16. ambaye sasa ana umri wa miaka 80. Pia ni siku chache tu kabla ya kusherehekea miaka miwili tangu Benediku 16. aliyechaguliwa madarakani. Tangu jana, sherehe za siku kuu hii zinafanyika mjini Roma.

Benedikt 16.

Benedikt 16.

Watu takriban 50.000 waliwasili kwenye uwanja wa mtakatifu Peter kule Vatika jana Jumapili kwa misa ya kusherehekea kuzaliwa Benedikt 16. Si kitu cha kawaida kuwa siku ya kuzaliwa kwake Baba Mtakatifu inasherehekewa rasmi kama mwaka huu. Siku kuu hasa ni siku ya kuchaguliwa Baba Mtakatifu. Kwa mujibu wa Vatikan, sababu ya sherehe kubwa juu ya Popu Benedikt 16. kufika umri wa miaka 80 ni kwamba watu, mashirika na maaskofu wengi walimuomba Baba huyu Mtakatifu kutoweka kando siku yake ya kuzaliwa.

Katika hotuba yake ya sherehe ya jana, Benedikt 16. waliwashuruku wageni na wajumbe wa kanisa wote, akitaja hasa wale walio karibu yake: “Ninamshuruku mungu kwamba nimeweza kufahamu uhumimu wa familia. Nimefahamu ubaba, maana yake mungu kuwa ni baba yetu kutokana na baba wangu wa kibindamu. Ninamshuruku mungu kwamba nimeweza kufahamu upole wa mama. Ninamshuruku mungu kwa dada na kaka yangu walionisaidia sana katika maisha yangu.”

Leo hii Benedikt 16. alipokea wageni wengi walimpongeza kwa siku ya kuzaliwa wakiwemo waziri mkuu wa mkoa wa Bavaria, Ujerumani, Bw. Edmund Stoiber. Mkoa huu ni nyumbani kwake Benedikt 16. ambapo alihudumia kama askofu. Kutoka Bavaria, Baba Benedikt pia alipata zawadi ya chupa 80 ya bia ya kibavaria kutoka kwa askofu wa Munich. Benedikt 16 lakini anajulikana kutopenda sana bia, badala yake anapenda chakula kitamukitamu, kwa hivyo amefurahia keki kutoka Ujerumani Kaskazini aliyoipewa na waziri mkuu wa mkoa wa Schleswig-Holstein. Meya wa mji wa Bonn ambapo Benedikt alisomesha kwenye chuo kikuu kwa miaka mitano alimpelekea Baba huyu Mtakatifu zaidi ya kadi 650 za pongeza zilizotengenezwa na watoto wa kanisa.

Wajerumani wengi wengine waumini walishiriki kwenye misa ya jana kwenye uwanja wa St. Peter na kumfurahisha Benedikt 16. Alisema: “Kwa furaha kubwa ninawasalimia waumini na wageni kutoka Ujerumani hapa kwenye uwanja wa St. Peter. Asante sana kwa kufika hapa. Ninaona bendera na nguo nyingi za Bavaria. Inagusa moyo wangu na ninafurahi.”

Mchana makardinali 50 walialikwa kwenye dhifa ya chakula cha mchana na baadaye jioni Baba Mtakatifu ameandaliwa burudani ya muziki.

 • Tarehe 16.04.2007
 • Mwandishi Maja Dreyer
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB4i
 • Tarehe 16.04.2007
 • Mwandishi Maja Dreyer
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB4i
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com