Serikali ya mseto yatangazwa Kenya. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 14.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Serikali ya mseto yatangazwa Kenya.

Rais Mwai Kibaki wa Kenya ametangaza baraza jipya la mawaziri 42.

default

Rais Mwai Kibaki wa Kenya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga hatimaye wameunda serikali y mseto.

NAIROBI:

Rais Mwai Kibaki  wa Kenya ametangaza baraza jipya la mawaziri 42 ikiwa ni hatua ya kumaliza mgogoro wa kisiasa uliokuwa  unaikabili Kenya kufuatia kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi  desemba  mwaka jana.

Rais Kibaki pia  amemtangaza  rasmi kiongozi wa upinzani wa chama cha ODM  Raila  Odinga kuwa waziri mkuu.

Akitangaza baraza hilo ikiwa ni hatua iliyofikiwa chini ya  makubaliano  ya kugawana  madaraka  na  upande  wa upinzani, bwana Kibaki amewataka wakenya  waweke kando  siasa  ili waanze kufanya  kazi ya kuijenga  nchi yao.

Katika baraza hilo,bwana uhuru Kenyatta wa  chama kinachotawala  PNU  na bwana Musalia Mudavadi wa  chama cha upinzani, ODM  watakuwa makamu wa waziri mkuu.

 • Tarehe 14.04.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DhBp
 • Tarehe 14.04.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DhBp
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com