1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Ripoti: Biashara za Trump zililipwa na serikali za kigeni

5 Januari 2024

Ripoti iliyochapishwa jana Alhamisi imesema baadhi ya serikali za kigeni zililipa kiasi cha dola milioni 7.8 kwenye biashara za Donald Trump wakati akiwa rais wa Marekani.

https://p.dw.com/p/4asDs
Donald Trump anakabiliwa na tuhuma mbalimbali zinazotishia kumzuia kuwania tena urais
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akipiga makofi katika moja ya mikutano yake ya kampeni uliofanyika huko Waterloo, Iowa, Desemba 19, 2023. Picha: Kamil Krzaczynski/AFP/Getty Images

Miongoni mwa serikali kwenye ripoti hiyo ya Kamati ya kusimamia Bunge linalodhibitiwa na chama cha Democrats ni pamoja na China, Saudi Arabia, India, Uturuki na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kulingana na ripoti hiyo, wawakilishi kutoka mataifa 20 walilipa fedha hizo kwenye hoteli za Trump na makampuni yake ya biashara za mali isiyohamishika wakati akiwa rais.

Waandishi wa ripoti hiyo wamedai kwamba mapato kama hayo kutoka serikali za kigeni yalikiuka zuio la kikatiba linalohusiana na malipo ya kigeni.