SAMARA: Merkel,Barroso na Putin wakutana Urusi | Habari za Ulimwengu | DW | 18.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SAMARA: Merkel,Barroso na Putin wakutana Urusi

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso wapo Samara kusini mwa Urusi kwa mazungumzo yasio rasmi pamoja na Rais Vladimir Putin wa Urusi. Merkel amekwenda kwa mazungumzo hayo,Ujerumani ikishika wadhifa wa urais wa Umoja wa Ulaya unaozunguka kila miezi sita.Majadiliano ya viongozi hao yana azma ya kupunguza mivutano iliyopo kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi,juu ya masuala mbali mbali.Mojawapo ya masuala hayo ni kupiga marufuku kwa Urusi,kuagizia nyama kutoka Poland na kuondoshwa kwa sanamu ya kumbukumbu ya vita ya enzi ya iliyokuwa Soviet Union,kutoka mji mkuu wa Estonia,Tallinn.Mipango ya kuanzisha majadiliano kuhusu mkataba wa ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi imeahirishwa kwa sababu ya mizozo ya hivi sasa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com