1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Safari za treni Ujerumani kuanza tena leo

13 Machi 2024

Shirika la reli la Ujerumani Deutsche Bahn lipo katika hatua ya kurejesha huduma zake za kawaida leo hii baada ya kumalizika kwa mgomo unaoratibiwa na Chama cha Madereva wa Treni GDL wa masaa 24, ulioanza jana.

https://p.dw.com/p/4dS8f
Mgomo wa madereva wa treni Ujerumani
Mgomo wa sita wa madereva wa treni Ujerumani huku majadiliano ya pamoja ya utatuzi wa mzozo huo yakiendelea, Stuttgart, Machi 11, 2024Picha: picture alliance/Panama Pictures

Msemaji wa shirika hilo, Achim Stauß amenukuliwa na vyombo vya habari akisema shirika hilo litaanza huduma zake haraka leo na kutoa huduma zake kwa ukamilifu.

Duru ya sita ya mgomo huo wa madereva wa treni uliathiri takribani asilimia 80 za treni za masafa marefu. Kiini cha mzozo ni madai ya madereva kutaka mabadiliko katika muda wa kazi, wakitaka kufanya kazi masaa 35, kwa malipo yaleyale ya  muda wa sasa wa masaa 38, pendekezo ambalo shirika la reli limeridhia kuingia katika majadiliano nao.