Ratiba ya michuano ya kandanda ya michezo ya Olimpik . | Michezo | DW | 20.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ratiba ya michuano ya kandanda ya michezo ya Olimpik .

Kura ya michuano ya kandanda wanaume katika michezo ijayo ya Olimpik imefanyika leo mjini Beijing, huku wenyeji China wakijikuta kundi C pamoja na Brazil, New Zealand na Ubeligiji. Katika mashindano hayo yatakayozishirikisha timu 16,amabingwa watetezi Argentina wako kundi A, wakiungana na Ivory Coast, Australia na Serbia. Kundi B ni waakilishi wengine wa Afrika Nigeria,wakiwa na Uholanzi, Japan, na marekaniv wakati Cameroun iko kundi D pamoja na Italia, Korea kusini na Honduras.

Katika kandanda la wanawake la michezo hiyo ya Olimpik China imepangwa kundi moja na Sweden, Argentina na Canada na mabingwa wa kombe la dunia wanawake, Ujerumani, na washindi wa pili Brazil wameangukia kundi la pamoja na Korea kaskazini na Nigeria.