1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin atishia kutumia nguvu endapo mazungumzo yatakwama

28 Desemba 2025

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Ukraine haina haraka ya kutafuta amani, na kwamba ikiwa haitaki kumaliza mzozo wao kwa njia ya amani, Moscow itatimiza malengo yake yote kwa kutumia nguvu.

https://p.dw.com/p/562Kw
Urusi 2025 | Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin atishia kutumia nguvu iwapo mazungumzo ya amani hayatofanikiwa.Picha: Vladimir Smirnov/TASS/ZUMA/picture alliance

Kauli ya Putin inajiri baada ya shambulio kubwa la droni na makombora kutoka Urusi, lililomfanya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kusema kuwa Urusi inaonyesha nia ya kuendeleza vita ilhali Kyiv inataka amani.

Zelenskiy anatarajiwa kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump huko Florida leo Jumapili kutafuta suluhisho la vita ambavyo Putin alivianzisha takriban miaka minne iliyopita.

Wakati huo huo, Urusi imedai kuiteka miji kadhaa katika mikoa ya Donetsk na Zaporizhzhia, madai ambayo Ukraine imeyakanusha, ikisema mapigano bado ni makali na operesheni za ulinzi zinaendelea.