1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin aonya juu ya kuwepo wanajeshi wa Ufaransa huko Ukraine

28 Mei 2024

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema Jumanne kuwa mamluki wa Ufaransa wamekuwa wakipigana vita upande wa Ukraine kwa muda mrefu.

https://p.dw.com/p/4gO74
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Mikhail Metzel/REUTERS

Ufaransa imekanusha madai ya Urusi kwamba imetuma mamluki nchini Ukraine, ingawa imeeleza kuwa haijaondoa uwezekano wa kutuma wakufunzi wa kijeshi katika siku za usoni japo bado haijafanya hivyo.

Jumatatu, Ukraine iliondoa tangazo lake kwamba wakufunzi wa kijeshi wa Ufaransa wangewasili nchini humo hivi karibuni na badala yake ikaeleza kuwa, bado inafanya mazungumzo na Ufaransa na washirika wake wengine juu ya suala hilo.