1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pompeo ashambulia sera za Obama mashariki ya kati

Sekione Kitojo
11 Januari 2019

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alimshutumu ais wa zamani wa Marekani Barack Obama kwa kupandikiza vurugu  kwa kulitelekeza eneo la mashariki ya kati kwa wanamgambo wa Kiislamu na ushawishi wa Iran. 

https://p.dw.com/p/3BMBH
Ägypten | Mike Pompeo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike PompeoPicha: picture-alliance/dpa/AP Photo/A. Nabil

Aliyasema  hayo katika ukosoaji  mkubwa  wa  sera  za  rais  huyo  wa  zamani  licha  ya hatua  za  mkuu  wa  Pompeo  rais Donald Trump  kuamua kuviondoa  vikosi vya  jeshi  la  Marekani  kutoka  Syria.

Ägypten | Mike Pompeo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo akihutubia katika chuo kikuu cha marekani mjini CairoPicha: picture-alliance/dpa/AP Photo/A. Nabil

Katika  bhotuba  ambayo  aliitoa  katika  chuo  kikuu  cha  Marekani mjini  Cairo, Pompeo  alijitenga  na utamaduni  wa  kidiplomasia  wa Marekani  wa  kuepuka kutangaza  hadharani  mizozo  wa  ndani nchini  Marekani  kwa  kumshambulia  Obama  katika  mahali ambapo  mtangulizi  huyo  wa  rais  Trum  alitoa  hotuba  ya kihistoria  yenye  lengo  la  kuimarisha  mahusiano  na  ulimwengu wa  Kiislamu. Pompeo ameiwasilisha  Marekani  kuwa  ni  nguvu  ya kufanya  mazuri  katika  mashariki  ya  kati,  na  kudokeza  kwamba Obama  aliiona  Marekani  kama " nguvu  inayoitaabisha  mashariki ya  kati".

"Tunahitaji  kutambua  ukweli  huu kwasababu  iwapo  hatutafanya hivyo, tutafanya  makosa  ya  uchaguzi. Kwa  hivi  sasa  na  hapo baadaye. Na uchaguzi  wetu , kile  tutakachokichagua  leo kina athari kwa  mataifa na  kwa  mamilioni  ya  watu , kwa  usalama  wetu, kwa ufanisi  wa  uchumi wetu, kwa  uhuru  wetu , na  ule  wa  watoto wetu."

Akosolewa

Baadhi  ya  maafisa  wa  zamani  wa  Marekani  na  wachambuzi wamemshutumu  mwanadiplomasia  huyo  wa  ngazi  ya  juu  wa Marekani  kwa  kusoma  vibaya  historia  na  kujificha  katika mapenzi  ya  binafsi  ya  Trump  kupunguza  jukumu  lake  katika eneo  hilo.

USA Barack Obama ehemaliger Präsident
rais wa zamani wa Marekani Barack Obama Picha: picture-alliance/dpa/O. Douliery

Pompeo  amemshutumu Obama  kwa kushindwa kupima  uwezo na ushupavu  wa  Uislamu  wa  itikadi  kali,"  na  kushindwa  kuunga mkono  kile  alichokiita  vuguvugu  la  kijani  la  maandamano  ya umma  kupinga  uchaguzi  uliobishaniwa  nchini  Iran, na  kutupia lawama  kwa  kutoishambulia  Syria  kwa  kulipiza  kisasi  kwa matumizi  ya  silaha  za  sumu  ya  majeshi  ya  serikali  katika  vita vya  wenyewe  kwa  wenyewe .

"Kitu  gani  tulijifunza  kutokana  na  hali  hii ?  Tumejifunza  kwamba wakati  Marekani  inajiweka  kando, machafuko  yanafuatia. Wakati tunawapuuza  marafiki, sononeko  la  chuki vinajijenga. Na  wakati tunashirikiana  na  maadui  zetu, wanasonga  mbele," Pompeo alisema.

USA Shutdown l Präsident Donald Trump wirbt in Texas für die Mauer
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Reuters/L. Millis

Pompeo  hakumtaja Obama  kwa  jina  lakini  alimuita  "Mmarekani mwingine"  ambaye  alitoa  hotuba  katika  mji wenye  wakaazi  wengi katika  mataifa  ya  Kiarabu . Ofisi  ya  Obama  ilikataa  kutoa maelezo  kuhusu  hotuba  hii.

Pompeo  anafanya  ziara  katika  eneo  hilo  kujaribu  kuelezea mkakati  wa  Marekani  baada  ya  tangazo  la  kushangaza  la Trump  mwezi  uliopita  la  kuwaondoa kwa  ghafla wanajeshi  2,000 wa  Marekani  kutoka  Syria, hatua  iliyowashangaza  washirika, kuwashitua  maafisa  wa  ngazi  ya  juu  wa  Marekani  na kusababisha  kujiuzulu  kwa  waziri  wa  ulinzi  wa  Marekani  Jim Mattis.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre

Mhariri: Josephat Charo