PARIS: Leo ni siku ya kumbukumbu ya utumwa duniani | Habari za Ulimwengu | DW | 23.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS: Leo ni siku ya kumbukumbu ya utumwa duniani

Leo ni siku ya kumbukumbu ya utumwa na kuangamizwa kwake duniani.

Katika hotuba yake mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia elimu, sayansi na utamaduni UNESCO bwana Koichira Matsuura amekumbusha juu ya utumwa ambao bado upo katika nyakati hizi.

Amehimiza watoto wafundishwe juu ya historia ya biashara ya watumwa ili wasisahau sura hiyo mbaya na pia kwa ajili ya kuwafunza watoto juu ya athari yake.

Nchini Uingereza katika mji wa Liverpool leo siku hii inadhimishwa kwa kufunguliwa rasmi jumba la kimataifa la makumbusho juu ya utumwa.

Mwaka huu ni mwaka wa 200 tangu Uingereza kupiga marufuku utumwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com