1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Papa Leo XIV, Mahmoud Abbas wajadili hali Mashariki ya kati

6 Novemba 2025

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo wa XIV amempokea rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmood Abbas Alhamisi huko Vatican, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu hali ya Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/53D16
Vatican
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Leo na Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud AbbasPicha: Vatican Media/IPA/ZUMA/dpa/picture alliance

Vatican imesema pande zote mbili zilikubaliana kwamba mzozo katika eneo hilo unaweza kumalizwa kupitia suluhu ya madola mawili yaani Palestina na Israel. Mkutano huo ni wa kwanza wa ana kwa ana kati ya Papa Leo na Abbas.

Umuhimu wa misaada ya kiutu waangaziwa

Wawili hao pia wamejadili hali katika Ukanda wa Gaza na kukubaliana kuhusu umuhimu wa kupelekwa misaada ya kiutu. Mahmoud Abbas, aliwahi kukutana na mtangulizi wa Papa Leo, Papa Francis mwezi Desemba mwaka uliopita.

Alichaguliwa kuwa kiongozi wa mamlaka hiyo mwaka 2005. Mamlaka hiyo inaendesha sehemu inayokaliwa kimabavu  na Israel ya Ukingo wa Magharibi, lakini ikapoteza udhibiti wa Ukanda wa Gaza, wakati Hamas walipoudhibiti mwaka 2007.