Ngono ili kupata samaki
Biashara ya samaki ni maarufu sana katika kujipatia kipato miongoni mwa wanawake wanaoishi eneo la Ziwa Viktoria. Lakini ili kupata samaki, wanawake hulazimika kuwalipia- na malipo yanayokubaliwa na wavuvi ni "ngono".
Ngono kwa ajili ya kupata samaki.
Wanawake wa Kenya huuza samaki kutoka katika ziwa Victoria katika masoko ya ndani. Kuuza samaki ni kawaida katika eneo hili ili kujiendesha kimaisha tangu miongo mingi iliyopita. Lakini ili kupata samaki hao, wanawake hulazimika kulipia - na sarafu iliyokubaliwa na wavuvi ni "ngono". Waandishi wa habari kutoka shirika la habari la Ujerumani dpa walikwenda Kenya kuzungumza na wanawake wahanga.
"Biashara ya Jaboya."
Perez Anjango aliuza samaki wakati akiwa mdogo. Kwa karibu miaka kumi na tano amekuwa sehemu ya biashara ambayo wakazi wa eneo hilo wanaiita"Jaboya" ama Kufanya ngono na wavuvi kama njia ya kupata samaki. Siku hizi mashirika kama World Vision yanajaribu kuwaonyesha wanawake jinsi ya kuepukana na "Jaboya".
Kukosekana usawa wa kijinsia ziwani.
Katika nyakati za asubuhi wavuvi hupeleka boti zao kuvua samaki - hii hufanywa na wanaume tu. Kuna ubaguzi mkubwa wa kijinsia katika biashara ya samaki kwenye eneo la ziwa Victoria.
Mmoja kati ya wengi.
Wakati wavuvi wanaporejea mapema asubuhi, tayari ufukwe huwa umejaa watu - hasa wanawake - wanaosubiri kupata samaki wao. Wavuvi huleta "dagaa", ambayo ni aina ya samaki inayouzwa sokoni hapo.
Mvuvi "halisi".
Wakati wavuvi wanapofika pwani, kila mwanamke anajua ni mashua ipi anayoilenga na wapi pa kupata ndoo yake ya plastiki iliyojazwa samaki. Ndoo moja ni sawa na kilo 35 za dagaa inayogharimi shilingi 1000 za Kenya ama euro 8,5. Ngono huja baadae, na hutolewa bure tu.
Watu wengi, samaki wachache sana.
Lakini inawezekanaje mvuvi akaweza kuwashawishi wanawake kujiingiza kwenye ukahaba? Jibu ni rahisi: Kwa sababu wanaweza kudai chochote wanachopenda ili kuwapatia samaki. Idadi ya watu katika eneo la ziwa huongezeka huku dagaa wakipungua sana ziwani kutokana na uchafuzi wa mazingira, uvuvi uliopitiliza juu ya jabali la Victoria, ilianzishwa ziwani hapo miaka ya 1950.
Kuwa rafiki mzuri zaidi.
Hivyo, ili kupata samaki wanawake wanapaswa kufanya "urafiki" na mvuvi. Hii inamaanisha watafanya ngono kabla au baada wanaume hawajakwenda kuvua. "Marafiki wazuri zaidi" wanaweza hata kupata samaki zaidi au wazuri zaidi kuliko wanawake wengine.
Tatizo la kusambaa kwa magonjwa.
Kinachotokea kwenye "Jaboya" sio tu nchini Kenya lakini pia katika nchi jirani za Uganda na Tanzania. Na hueneza magonjwa katika eneo la ziwa: viwango vya maambukizi ya VVU viko juu hasa kwenye ukanda huo, na kuua wanawake na wavuvi ambao huacha wake wao wajane, tena bila ya kipato.
Vyanzo vipya vya mapato:
Ni vigumu kuiepuka biashara ya "Jaboya": Kwanza wanawake hupaswa kupata kazi nyingine. Mashirika kama "World Vision" yanawaonyesha njia mpya za kujipatia pesa. Mwanamke huyu hutengeneza majiko ya kuokea kwa udongo wa ufinyanzi huko Sindo, ambao ni mji mdogo ulio karibu na ziwa.
Kuanzisha biashara nzuri.
Perez Anjango na familia yake hivi sasa wana bwawa la kuzalisha samaki wenyewe: Bwawa lake lina ukubwa wa nusu ya uwanja wa mpura wa tenisi, na lipo karibu na ziwa Victoria. Mmoja wa binti Anjangos huuza samaki sokoni - lakini daima hukaa mbali na ufukwe.