New York.Mvutano bado waendelea katika kutafuta kiti cha Amerika ya kusini. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

New York.Mvutano bado waendelea katika kutafuta kiti cha Amerika ya kusini.

Mvutano juu ya kiti cha Amerika ya Kusini katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bado unaendelea.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limeakhirisha upigaji kura kwa muda wa siku tano, baada ya chaguzi nyengine sita kushindwa kupata mshindi kati ya Guatemala inayoungwa mkono na Marekani na Venezuela.

Wanadiplomasia wamesema kwamba, mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi zote mbili watakutana hii leo ili kujaribu kutafuta suluhisho la mvutano huo.

Rais wa Venezuela hugo Chavez amependekeza kwamba Bolivia ichaguliwe kama mtetezi wa kumaliza mvutano huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com