NEW YORK: Mashambulizi ya Irak yalaaniwa vikali
17 Agosti 2007Matangazo
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mashambulizi manne yaliyofanywa kwa wakati mmoja,kaskazini mwa Irak.Mashambulizi hayo ya kujitolea muhanga yameua watu wasiopungua 400. Taarifa iliyotolewa na baraza hilo imesema,azma ya mashambulizi hayo ni kuzitenga zaidi jamii za kidini na kikabila nchini Irak.
Mashambulio hayo yalilenga vijiji wanakoishi waumini wa madhehebu ya kale ya Yazidi na yamesababisha idadi kubwa sana ya vifo.