New York. Leo ni siku ya ukimwi duniani. | Habari za Ulimwengu | DW | 01.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

New York. Leo ni siku ya ukimwi duniani.

Siku ya ukimwi duniani inaadhimishwa duniani kote leo wakati ugonjwa huo ukiendelea kuleta maafa, na watu wanaokadiriwa kufikia milioni nne wakiambukizwa virusi vya HIV kila mwaka.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amewataka watu kuendelea na mapambano dhidi ya ukimwi, akiongeza kuwa wanasiasa wanapaswa kuwajibika.

Katika sherehe za maadhimisho hayo mjini New York , Annan amesema kuwa virusi vya ukimwi, ambavyo vimeuwa watu zaidi ya milioni 25 na kuambukiza watu milioni 40 zaidi, ni changamoto kubwa katika enzi zetu.

Eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara linabaki kuwa ndio eneo lililoathirika zaidi, likiwa na watu milioni 24.7 walioathirika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com