1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Blair kushughulikia Mashariki ya Kati

28 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBng

Aliekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza,Tony Blair ameteuliwa kama mjumbe mpya wa kundi la pande nne linalotafuta suluhisho la amani katika Mashariki ya Kati.Umoja wa Mataifa ulitoa tangazo hilo muda mfupi baada ya Urusi kuondosha upinzani wake kuhusika na uteuzi wa Blair.Kundi la pande nne hufungamanisha Umoja wa Ulaya,Urusi,Marekani na Umoja wa Mataifa.Inatumainiwa kuwa Blair ataufufua mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati uliokwama.Tony Blair amesema,yeye anataka kushughulikia kile kinachojulikana kama “suluhisho la mataifa mawili“ yaani kuundwa taifa la Palestina litakalotambuliwa kimataifa,likiwa kando ya Israel.