NAIROBI: Polisi Kenya yakanusha kuhusika na mauaji ya washukiwa Mungiki | Habari za Ulimwengu | DW | 07.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI: Polisi Kenya yakanusha kuhusika na mauaji ya washukiwa Mungiki

Polisi nchini Kenya wamekanusha tuhuma kuwa wameua takriban watu 500 walioshukiwa kuwa wanachama wa kundi halifu la Mungiki.Madai hayo yametolewa na Halmashauri ya Kenya kuhusika na Haki za Binadamu(KNCHR),baada ya kutoweka kwa wanachama wa Mungiki.Kundi hilo halifu,mapema mwaka huu lilisababisha fujo na vitisho katika baadi ya maeneo ya mji mkuu Nairobi.

Maiti za mamia ya watu,zimekutikana katika nyumba ya maiti mjini Nairobi.Kwa mujibu wa KNCHR,maiti hizo zina alama zinazoashiria kuwa watu hao waliuawa,kwa hivyo inaaminiwa kuwa ni polisi waliohusika.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com