1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Namatai Kwekweza ashinda tuzo ya juu ya heshima Ujerumani

27 Novemba 2025

Ujerumani imemtunuku tuzo ya juu ya heshima kwa Afrika mwanaharakati wa Zimbabwe Namatai Kwekweza. Tuzo hiyo ni kutokana na ujasiri na dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha utawala wa sheria na demokrasia nchini mwake.

https://p.dw.com/p/54OEh
Kwekweza ametunukiwa tuzo ya juu ya heshima ya Ujerumani kwa Afrika kwa mwaka 2025
Mwanaharakati kijana wa Zimbabwe Namatai KwekwezaPicha: Privilege Musvanhiri/DW

Mwanaharakati huyo mwenye miaka 26 alichaguliwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2025 na jopo la majaji 20 kati ya zaidi ya washiriki 20 waliowania tuzo hiyo. Jopo hilo huru limeeleza kuwa juhudi za Kwekweza zinatoa ujumbe wa kujiamini na kufufua demokrasia.

Rais wa Bunge la Ujerumani ampongeza Kwekweza

Katika hafla maalumu ya kutoa tuzo hiyo iliyofanyika Jumatano mjini Berlin, Rais wa bunge la Ujerumani Julia Klöckner alimsifu raia huyo wa Zimbabwe  kwa kutumia nafasi yake kuhubiri demokrasia na utawala wa sheria nchini Zimbabwe.

Namatai Kwekweza ni mwanzilishi wa shirika la WELEAD Trust, linalotoa mafunzo kwa viongozi vijana na linawashirikisha katika michakato ya maamuzi ya kisiasa.