Muda unayoyoma Marekani
31 Julai 2011Matangazo
Wanachama wa republican pia wanasema wamo katika mazungumzo muhimu na wana imani ya kufikia makubaliano. Mabaraza yote ya wawakilishi na seneti ambayo yanaongozwa na vyama hasimu, yamepinga mapendekezo yaliyowasilishwa. Rais Obama anaetaka kuumaliza mjadala huo wa deni la nchi hiyo, hapo jana, alisisitiza mwito wake kwa pande zote kuafikiana.
Marekani ina mpaka saa sita usiku Jumanne, kufikia makubaliano ya kupandisha kiwango cha deni la nchi hiyo, la sivyo itashindwa kulipa madeni yake, hali itakayoweza kuathiri vibaya uchumi duniani.
Mwandishi: Maryam Abdalla/afp rtr cnn dwtv
Mhariri:Martin, Prema