1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msemaji wa walinzi wa mapinduzi wa kiislamu wa Iran auliwa

Josephat Charo
20 Machi 2026

Msemaji wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi ya kiislamu cha Iran (IRGC), Ali Mohammad Naini, ameuawa katika shambulio.

https://p.dw.com/p/5Ao03
Msemaji wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi ya kiislamu cha Iran Ali Mohammad Naini, ameuawa.
Msemaji wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi ya kiislamu cha Iran Ali Mohammad Naini, ameuawa.Picha: Tasnim

Msemaji wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi ya kiislamu cha Iran (IRGC), Ali Mohammad Naini, ameuawa katika shambulio.

Shirika la habari la Tasnim, ambalo liko karibu na kikosi hicho maalumu, limeripoti kwamba jenerali huyo aliuawa katika shambulio ambalo IRGC imezinyoshea kidole cha lawama Israeli na Marekani. Naini alielezewa kama kamanda mkongwe ambaye alikuwa ameitumikia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa zaidi ya miongo minne.

Wakati haya yakiarifiwa, msemaji mkuu wa jeshi la Iran ameonya kwamba mabustani, maeneo ya burudani na sehemu za watalii duniani kote hazitakuwa salama kwa maadui wa Tehran.

Jenerali Abolfazl Shekarchi ametoa tishio hilo leo Ijumaa huku Iran ikiendelea kushambuliwa na mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel.