Mpango wa nuklia na Urusi sio halali | Matukio ya Afrika | DW | 27.04.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Mpango wa nuklia na Urusi sio halali

Mahakama kuu Afrika Kusini imetangaza kuwa mkataba wa Afrika Kusini na kampuni moja ya Urusi kuhusu Nyuklia sio halali

Mkataba wa Afrika Kusini na kampuni ya Rosatom ya Urusi kujenga vinu vya nyuklia umetangazwa kuwa uko kinyume na sheria na mahakama kuu siku ya Jumatano 26.04.2017 na kuweka mashaka mapya juu ya mipango ya nishati ya nchi hiyo.

Kampuni pekee yenye kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za nyuklia barani Afrika Eskom inataka kuongeza megawati 9,600 ya uwezo wa nyuklia sawa na vinu 19 vya kuzalisha umeme kwa nguvu hizo za nyuklia kusaidia uchumi kuacha kutegmea makaa ya mawe katika kile kiliweza kuwa kandarasi kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa duniani kwa miongo mingi.

Afrika Kusini na Urusi zimesaini makubaliano ya kiserikali hapo mwaka 2014 ambayo yameidhinisha ushirikiano kati ya kampuni  ya shughuli za nyuklia Rosatorm na ile ya umeme inayomilikiwa na serikali ya Eskom.

Jaji Lee Bozalek amesema ombi lililotolewa la kutaka taarifa za kuanza mchakato wa mkataba huo limewekwa kando  sawa na mkataba wenyewe wa ushirikiano.

 

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com