MONTEBELLO: Rais Bush akiri kutorodhishwa na serikali ya Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 22.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MONTEBELLO: Rais Bush akiri kutorodhishwa na serikali ya Irak

Rais George W Bush wa Marekani amekiri kutoridhishwa na serikali ya Irak. Bush ameyasema hayo katika mkutano na viongozi wa Marekani mjini Montebello, Kanada.

Balozi wa Marekani nchini Irak Ryan Crocker ameulaumu utawala wa waziri mkuu wa Irak Nouri al Malik kwa kutotia bidii kupambana na hali ya machafuko na pia kuzorota katika kutafuta suluhu ya kitaifa. Bwana Crocker amesema serikali ya Marekani imevunjwa moyo sana kutokana hali hiyo.

Rais Bush amesema ikiwa serikali ya Irak itashindwa kutimiza madai ya raia wake basi wananchi wataiondoa serikali hiyo kutoka madarakani.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bernard Kouchcner amesema kwamba bara la Ulaya lazima liwajibike kwa kiwango kikubwa katika kutatua matatizo yanayoikabili Irak kwa sababu Marekani haiwezi haitaweza kutimiza jukumu hilo peke yake.

Kouchner ni afisa wa kwanza wa ngazi ya juu wa Ufaransa kuzuru Irak tangu serikali ya Saddam Hussein ilipong’olewa katika uvamizi ulio ongozwa na Marekani mwaka 2003.

Wakati huo huo wanajeshi 14 wa marekani wameuwawa katika ajali ya helikopta kaskazini mwa Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com