Mkutano wa ulinzi wa viumbe na mazingira wafunguliwa leo Bonn. | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 19.05.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Mkutano wa ulinzi wa viumbe na mazingira wafunguliwa leo Bonn.

Mkutano wa nne wa Umoja wa Mataifa juu ya kulinda viumbe na mazingira yaliyomo katika hatari ya kutoeka umefunguliwa leo mjini Bonn na waziri wa mazingira wa Ujerumani bwana Sigmar Gabriel.

Waziri wa mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel akifungua mkutano juu ya ulinzi wa mazingira mjini Bonn .

Waziri wa mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel akifungua mkutano juu ya ulinzi wa mazingira mjini Bonn .

Waziri wa ulinzi wa mazingira wa Ujerumani bwana Sigmar Gabriel ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa juu ya kuchukua hatua za haraka ili kuepusha kuteketezwa viumbe na mazingira. Waziri Gabriel amesema dunia sasa imefikia mahala pabaya ambapo mazingira na mimea ya aina mbalimbali inatoeka kwa haraka.

Waziri Gabriel amesema hayo katika hotuba yake ya kufungua mkutano juu ya kulinda viumbe na mazingira yalimo hatarini kutoeka unaofanyika mjini Bonn nchini Ujerumani.

Mkutano huo wa siku tisa unahudhuriwa na wajumbe wapatao 6000 kutoka nchi 190.

Katika juhudi za kupambana na hatari ya mazingira na viumbe vya aina mbalimbali kutokomea kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kutangaza nyongeza ya fedha kwa ajili ya kusaidia juhudi hizo.

Mkutano huo wa nne unaofanyika chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa na uenyekiti wa Ujerumani unajadili njia za ufanisi za kupambana na hatari zinazotishia maeneo kama misitu muhimu na viumbe mbalimbali duniani.
 • Tarehe 19.05.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E2Qj
 • Tarehe 19.05.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E2Qj
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com