Mkutano wa tabia nchi magazetini | Magazetini | DW | 18.11.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Mkutano wa tabia nchi magazetini

Mkutano wa tabia nchi,mazungumzo ya kuunda serikali kuu ya muungano na hali ya eneo la mashariki ya Ujerumani miaka 25 baada ya ukuta wa Berlin kuporomoka ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa zaidi magazetini

Wanahjarakati wa shirika la ulinzi wa mazingira.Green Peace wanaandamana mbele ya mgodi wa makaa mawe huko Belchatow nchini Poland

Wanahjarakati wa shirika la ulinzi wa mazingira.Green Peace wanaandamana mbele ya mgodi wa makaa mawe huko Belchatow nchini Poland

Tuanzie Warsaw unakoendelea mkutano wa kimataifa wa tabia nchi.Gazeti la "Stuttgarter Nachrichten linajiuliza?

Kwanini mazungumzo ya kusaka makubaliano timamu ya tabia nchi yanazorota?Kwanini wataalamu wanaonekana kama watu waliolazimishwa kushiriki katika mazungumzo ya Warsaw?Sababu ni dhahiri,matokeo ya kutofanya chochote yatakuwa na madhara ambayo binaadamu hawajawahi kuyashuhudia hadi sasa.Ukweli ni kwamba:wanasiasa wanaonyesha wanashindwa kuona mbali.Kwasababu kitakachopitishwa leo kitavisaidia kwanza vizazi vijavyo.Kwasasa watu wanaonyesha kupakata mikono.Ujerumani,inayoshika usukani kutokana na nguvu zake za kiuchumi ndani ya Umoja wa Ulaya haifanyi chochote kikubwa.Angalieni mpango wa kuifanyia merekebisho sekta ya nishati.Mpango huo ambao awali ulikuwa ukiangaliwa kama ngao ya kujikinga dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi,unatiwa ila badala ya kuzingatiwa.

Mazungumzo ya kuunda serikali kuu ya muungano kati ya vyama ndugu vya Christian Democratic Union-CDU,Christian Social Union CSU na wasocial Democratic wa SPD yameingia awamu muhimu,huku watu wakianza kujiuliza kama kweli mazungumzo hayo yataleta tija.Gazeti la "Landeszeitung" la mjini Lüneberg linaandika:

SPD na CDU/CSU wametangaza kuweka kando usuhuba.Hiyo inamaanisha mazungumzo ya kuunda serikali kuu ya muungano yameingia awamu ngumu.SPD wanajitosa.Na licha ya matokeo dhaifu ya uchaguzi mkuu,hawana karata mbaya.Mwenyekiti wao Sigmar Gabriel anatambua,vyama ndugu vya CDU/CSU vinataka kuendelea kuwepo madarakani.Na anajua pia kwamba walinzi wa mazingira,hawafikirii kuwa washirika serikalini.Kwa hivyo anazidisha masharti ya kujiunga katika serikali ya muungano wa vyama vikuu.Sio tu kiwango cha chini cha mshahara kwa wote,hivi sasa anadai pia likubaliwe suala la uraia wa nchi mbili.Vyama ndugu vya CDU/CSU vinabidi viridhie la sivyo shina la SPD litapinga mkataba wa muungano.Kwamba hatima yake mwenyewe Gabriel kama mwenyekiti wa SPD itaingia hatarini,hilo halimshughulishi.

Ripoti yetu ya mwisho magazetini hii leo inahusu ujenzi wa eneo la mashariki ya Ujerumani.Gazeti la "Märkische Allgemeine" linaandika:

"Mtungi uko shina."Katika kipindi cha robo karne iliyopita,tangu ukuta wa Berlin ulipoanguka,majimbo mepya yamepiga hatua ambayo wengi wakati ule hawakuwa wakitarajia."Mandhari yananawiri" kama alivyoahidi Helmut Kohl mnamo siku ya kuungana sarafu za pande mbili za Ujerumani.Lakini pia kuna kasoro zinazobiri kusawazishwa kati ya maeneo ya mashariki na magharibi naiwe upande wa mishahara,malipo ya uzeeni na nyenginezo.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Yusuf Saumu