Misri kuufunga mpaka wake na Gaza leo | Habari za Ulimwengu | DW | 25.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Misri kuufunga mpaka wake na Gaza leo

Misri leo inajiandaa kuufunga mpaka wake na Gaza baada ya Marekani kuitaka izuie wimbi kubwa la watu ambao wamekuwa wakivuka mpaka katika siku tatu zilizopita.

Maafisa wa usalama wa Misri wametangaza kutumia kipaza sauti katika miji iliyo karibu na Ukanda wa Gaza kwamba eneo hilo huenda likafungwa kuanzia leo mchana, huku idadi isiyojulikana ya wapalestina wakiwa bado nchini Misri.

Wanamgambo wanne wa kundi la Hamas wameuwawa leo kwenye mashambulio ya angani yaliyofanywa na jeshi la Israel mjini Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Msemaji wa jeshi la Israel amethibitisha mashambulio hayo dhidi ya motokaa zilizokuwa zimewabeba makamanda wa kundi la al Qassam ambalo ni kitengo cha kijeshi cha kundi la Hamas.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com