Misri inapanga kuifunga mipaka na Gaza | Matukio ya Kisiasa | DW | 25.01.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Misri inapanga kuifunga mipaka na Gaza

Wapalastina wanazidi kumiminika Rafah licha ya uamuzi wa Misri wa kuifunga mipaka yake na Gaza

default

Wapalastina wakibeba vyakula toka Rafah kuerejea nyumbani GazaVikosi vya usalama vya Misri vimepewa amri ya kuzuwia mikururo ya malaki ya wapalastina  wa Gaza wanaomiminika Rafah na El Arich tangu jumatano iliyopita.MIpaka ya Misri itafungwa leo alasiri.


 Vikosi vya usalama vya Misri vimewekwa katika lango la Salahdin-eneo la mpakani wanakopitia wapalastina wengi wanaoingia Misri tangu ukuta na senyenge zilipovunjwa jumatano iliyopita.


Wanazuwiya,bila ya kutumia nguvu,wapalastina wasizidi kuvuka mpaka katika wakati ambapo maelfu ya wenzao wanarejea kwa khiari Gaza wakibeba bidhaa walizonunua upande wa pili wa mji wa Rafah-katika ardhi ya Misri au katika mji mwengine wa mpakani El Arich pia nchini Misri.


Hata hiovyo wapalastina wanaendelea kuingia Misri bila ya hofu yoyote baada ya-kuvunja vizuwizi vyengine vya mpakani.


Mashahidi na duru za polisi ya Hamas wamethibitisha kwamba maafisa wa Misri wameweka vizuwizi kuwazuwia wapalastina wasiingie El Anrich kutoka Rafah.


Hatua za usalama za misri zinatarajiwa kuimarishwa na maeneo ya mpakani kufungwa kuanzia laasiri ya leo.


Kabla ya hapo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani bibi Condoleezza Rice alisema ni jukumu la Misri kudhamini usalama katika eneo la mpakani pamoja na Gaza. Bibi Condoleewzzaq Rice amesema tunanukuu:"Hali ni ngumu kwao,inaeleweka,lakini huu ni mpaka wa kimataifa,unabidi ulindwe"Mwisho wa kumnukuu.


Kwa upande wake katibu mkuu wa jumuia ya nchi za kiarabu Amr Musa anasema:


"Wapalastina wangeona dalili mambo yanaanza kubadilika,naamini msimamo wao ungekua mwengine.Tunachokishuhudia hivi sasa ni matokeo ya kuvunjika moyo,hasira na kutokua na matumaini kwamba hali yao ya maisha itabadilika na lengo lao litafikiwa.Tunataraji tija itapatikana."


Israel imezungumzia azma ya kuiachia Misri dhamana ya kuwashughulikia wakaazi wa Gaza.Naibu waziri wa ulinzi wa Israel Matan Vilnai amesema jana nchi yake inaachana na eneo hilo la mwambao wanakoishi zaidi ya wapalastina milioni moja na nusu.Israel- ilikongoa maeneo ya wahamiaji wa kiyahudi na kuwaondowa wanajeshi wake Gaza tangu mwaka 2005,ingawa wanajeshi wa Israel wanaendelea kuikagua mipaka ya eneo hilo. Wadadisi wanaamini tangazo la Israel la kuachana na Gaza linahusu zaidi kusitisha juhudi za kuwapatia nishati,maji na madawa.


Wakati huo huo wapalastina  zaidi ya watano-wanaosemekana kua wanaharakati wa Hamas, wameuliwa Rafah madege ya Israel yalipotupa mabomu dhidi ya gari yao kusini mwa Gaza.


Na polisi wa Israel wamewekwa katika hali ya tahadhari hii leo Mashariki ya Jerusalem,pakihofiwa kuzuka machafuko baada ya Sala ya ijumaa.

 • Tarehe 25.01.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CxUb
 • Tarehe 25.01.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CxUb
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com