1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mikakati ya Marekani kwa Afrika ni fursa au kizingiti?

Angela Mdungu /Martina Schwikowski
12 Desemba 2025

Katika sera yake mpya ya mambo ya kigeni na mkakati wa kiuchumi Marekani, Ni wazi kwamba Rais Donald Trump halipi kipaumbele swala la miradi ya maendeleo Afrika ila anacholenga ni kupata malighafi na miradi ya nishati.

https://p.dw.com/p/55GIx
USA Palm Beach 2025 | Donald Trump spricht nach Schuss auf Nationalgardisten in Washington
Picha: Daniel Torok/Avalon/Photoshot/picture alliance

Kwa mujibu wa chapisho la Desemba 4 mwaka huu, Marekani inataka kufanya kazi hapo baadaye na nchi chache ilizozichagua ili kukuza "uhusiano wa kibiashara wenye maslahi kwa wote" na kujipatia rasilimali za Afrika na vitu vyenye manufaa kiuchumi, gesi oevu ya petroli na teknolojia nyingine zinazoweza kutumiwa Afrika.

Suala muhimu la kufikirisha ni kama mipango hii ya Trump ya kuihusisha Afrika kama msambazaji mkuu wa malighafi muhimu inaweza pia kutoa fursa mpya kwa maendeleo ya bara hilo japokuwa mchambuzi wa masuala ya Uchumi kutoka Kenya James Shikwati ana wasiwasi kuhusu hilo:

 "Sera ya usalama ya Marekani inaichukulia Afrika kama eneo ambalo sio la umuhimu. Ni wazi kuwa mkakati wa Trump unakinzana na matarajio ya Umoja wa Afrika na jumuiya nyingine za Uchumi barani Afrika ambayo ni kuunganisha uchumi wa kanda yote na kuifanya Afrika ijiendeshe ikiwa kitu kimoja".

Shikwati anasisitiza kuwa mbinu hii mpya ya Marekani haitoi nafasi yoyote kwa Afrika kujijenga upya. Zaidi anasema huenda ikaongeza idadi ya mizozo hasa ya kuwania rasilimali.

Baadhi wanaona ushirikiano mpya wa kiuchumi kuwa fursa kwa Afrika

Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa barani Africa UNDP Bi Ahunna Eziakonwa, ana mtazamo tofauti kwani anauona ushirikiano huu mpya wa kiuchumi kuwa fursa kwa Afrika kujiendeleza zaidi ili mradi tu uwe ushirika wenye kuleta maendeleo.

Hata hivyo hakuna dalili za msaada wa maendeleo kutoka Marekani. Itakumbukwa kuwa Trump aliisitisha misaada mwanzoni kabisa mwa muhula wake na kulifutnga shirika la Marekani la Misaada ya Kimataifa USAID.

Afrika Kusini  | African Growth and Opportunity Act | AGOA
Rais wa Afrika Kusini Cyril RamaphosaPicha: SIPHIWE SIBEKO/REUTERS

Itakumbukwa kuwa mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka 2025 kiongozi huyo aliupa kisogo kwa kutouongezea muda mpango wa biashara wa AGOA. Mradi huu uliozinduliwa mwaka wa 2000 uliziwezesha nchi nyingi za Afrika kupeleka bidhaa zao kwenye soko la Marekani bila kutozwa ushuru. Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama aliuona mradi huo kuwa muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Afrikana kuuongezea muda wa miaka mingine kumi baada ya kufikia kikomo mwaka 2015

Kijiografia hata hivyo Afrika inabeba jukumu kubwa kwa Marekani kwasababu ni adui mkubwa wa China ambayo imepata mafanikio makubwa barani humo. Mkakati wa Marekani unaibua uwezekano wa kuhusishwa katika usuluhishi wa mizozo japokuwa wataalamu wanasema kwa sasa umakini mkubwa umeelekezwa kwenye malighafi.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni mfano mzuri wa nguvu ya kisiasa ya Marekani. Trump anajinasibu kama msuluhishi wa mzozo kati ya Rwanda na Kongo.

Japokuwa alisimamia makubaliano ya amani Juni mwaka huu, mapigano mapya yanaendelea kuibuka katika eneo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali mashariki mwa Kongo. Mtaalamu wa masuala ya Afrika Robert Kappel, anasema nchi zilizojaribu kuipinga Marekani kama vile Afrika Kusini zinapigwa vita.