Michuano ya CECAFA yapamba moto | Michezo | DW | 24.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Michuano ya CECAFA yapamba moto

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati - CECAFA Senior Challenge inaendelea kupamba moto katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa

Malawi ambayo inashiriki kama timu ya kualikwa, imepata ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Sudan. Katika mchuano mwingine wa jana Jumatatu, Sudan Kusini iliichapa Djibouti 2-0.

Leo Jumanne, Zanzibar Heroes watashuka dimbani na Uganda. Tanzania Bara, maarufu kama Kilimanjaro Stars watakuwa wageni wa Rwanda.

Kenya, walianza vizuri kampeni yao baada ya kuwaangusha mahasimu wao wakubwa Uganda kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kundi B. Kenya iko sawa kwa pointi na Burundi, baada ya Burundi kuishinda Zanzibar kwa bao 1- 0. Nayo Rwanda ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Ethiopia, na Tanzania bara ikaishinda Somalia kwa mabao 4-0 katika kundi A.

Mwandishi: Sekione Kitojo/AFP
Mhariri: Bruce Amani

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com