1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfanyabiashara wa Iran akamatwa Ujerumani

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVtB

BERLIN.Mfanyabiashara mmoja raia wa Iran amekamatwa nchini Ujerumani akishukiwa kupeleka nchini mwake malighafi ambazo zinaweza kutumika kutengeza silaha la nuklia.

Kwa mujibu wa gazeti la hapa Ujerumani la kila wiki la Der Spiegel, polisi walimkamata mtu huyo aliyetambuliwa kwa jina la Mohsen Jumanne wiki iliyopita mjini Frankfurt.

Gazeti hilo limesema kuwa mtu huyo pia anatuhumiwa kuingiza nchini Iran aina ya pump kutoka Marekani pamoja na Camera za Kirusi vitu ambavyo hutumika katika utafiti wa nuklia.