Matumaini ya amani ya mashariki ya kati | Habari za Ulimwengu | DW | 29.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Matumaini ya amani ya mashariki ya kati

Jerusalem:

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema katika mahojiano na gazeti la Haaretz,kuundwa dola la Palastina litakaloishi kwa amani pamoja na Israel ni muhimu kwao.“Waziri mkuu wa Israel ameashiria uwezekano wa kuzuka mapambano kama yale yaliyoshuhudiwa Afrika kusini ya zamani ya kupigania haki ya kupiga kura- moja mtu mmoja,ikiwa anasema ufumbuzi wa madola mawili utashindikana.Na hali kama hiyo ikizuka anasema,itamaanisha tunanukuu:mwisho wa taifa la Israel-Mwisho wa kumnukuu waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert.Wakati huo huo balozi wa Syria nchini Ujerumani Hussein Omran anahisi amani ya kudumu lazma ijumuishe suala la Golam.Balozi Omran anaendelea kusema:

“Kwetu sisi bila ya shaka ni jambo muhimu kabisa ufumbuzi wa m zozo jumla ujumuishe pia kurejeshewa Syria ardhi yake-milima ya Golan.Hatuwezi kattu kuachia madai hayo.Hilo kwangu mie ni sharti la lazima,ili amani iweze kua jumla kwasababu ukitaka kutatua sehemu ya tatizo na mengine sio tuu unayaacha kando,lakini unayapuuza pia,hapo kuna hatari kwamba hali ya utulivu haitaweza kupatikana.Bila ya árdhi,nionavyo mie hakutakua na amani.”

Waisrael na Wapalastina wamekubaliana kuanzisha mazungumzo yatakayopelekea kupatikana makubaliano ya amani hadi ifikapo mwisho wa mwaka 2008.

 • Tarehe 29.11.2007
 • Mwandishi Oumilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CUiF
 • Tarehe 29.11.2007
 • Mwandishi Oumilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CUiF
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com