Mashirika ya misaada yatahadharisha juu ya kuzuka maradhi A.Kusini | Habari za Ulimwengu | DW | 24.05.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mashirika ya misaada yatahadharisha juu ya kuzuka maradhi A.Kusini

-

PRETORIA

Mashirika ya misaada yameonya kwamba wimbi linaloendelea la mashmbulio ya chuki dhidi ya wahamiaji nchini Afrika Kusini

linayaweka hatarini maisha ya maelfu ya wakimbizi kufuatia kitisho cha kuzuka kwa maradhi.Shirika la madaktari wasiojali mipaka limesema kuwa watu huenda wakaambukizwa maradhi kutokana na kujaa kupita kiasi makambi ya wakimbizi.Maelfu ya watu wanakimbilia kambi hizo kutokana na kuenea ghasia hizo ambazo zimeingia hadi Cape Town mji wa pili kwa ukubwa nchini humo.Hapo jana Afrika Kusini iliomba radhi kwa mara ya kwanza hadharani juu ya ghasia hizo ambazo zimesababisha kuuwawa kiasi cha watu 42 tangu zilipoanza zaidi ya wiki moja sasa.Wengi walioathirioka na ghasia hizo ni wakimbizi kutoka Zimbabwe,Malawi na Msumbiji pamoja na jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Aidha wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika waliokuwa wakikutana Arusha Tz walieleza kufadhaishwa kwao na mauaji hayo dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com