Maroketi yashambulia makazi ya Rais Saleh
4 Juni 2011Matangazo
Watu 7 wameuawa katika shambulio hilo mjini Sanaa. Waziri Mkuu na Spika wa Bunge ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa. Rais Saleh, amesema kuwa yeye ni mzima na amelilaumu kundi la kikabila kwa mashambulizi hayo.Sheikh Sadiq al-Ahmar, anaeongoza muungano wa kikabila unaotaka kumuondoa Saleh madarakani, amekana kuhusika na shambulio hilo.
Nae Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amesema, kuna mpango wa kuwahamisha raia wa umoja huo kutoka Yemen kwa sababu ya machafuko yanayozidi kushika kasi nchini humo.