Marekani yawasihi waafrika wamshinikize Gaddafi ang'atuke
10 Agosti 2011Balozi wa zamani wa Marekani nchini Libya Gene Cretz na afisa mmoja wa ngazi ya juu wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani Donald Yamamoto wamewasili katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa tangu jumatatu iliyopita.
"Wanadiplomasia hao wamekwenda Afrika kwa lengo la kuzungumza na wanachama wa Umoja wa Afrika kuhusu mgogoro wa Libya na umuhimu wa kumuona Gaddafi aking'oka madarakani-" amesema hayo msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani Mark Toner mjini Washington.
Wanadiplomasia hao wawili wameshazungumza na waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi na walipangiwa kuonana na mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Jean Ping kabla ya kuondoka Addis Ababa hapo jana.Walizungumza pia na kiongozi wa pili wa waasi wa Libya,Mahmoud Djibril ambae pia yuko ziarani nchini Ethiopia.
Marekani imeliruhusu baraza la mpito lililoundwa na waasi nchini Libya kukalia kukalia ubalozi wa Libya mjini Washington.Ubalozi huo ulifungwa na serikali bya Washington tangu March kumi iliyopita.Marekani imelitambua baraza la mpito la waasi kuwa ndio" uongozi halali unaodhibiti serikali nchini Libya".
Wakati huo huo serikali ya Libya imeituhumu jumuia ya kujihami ya NATO kuwauwa watu 85 madege yake ya kivita yalipotupa mabomu katika kijiji cha mashariki ,umbali wa kilomita kama 10 hivi kusini mwa mji unaogombaniwa wa Zliten.
Msemaji wa serikali ya Libya,Musa Ibrahim anasema:
"Raia 85,ikiwa ni pamoja nawaatoto 35,wanaume 20 na wanawake 32 wameuliwa,na bado tunaendelea kuhesabu idadi ya wahanga wa mashambulio makali ya madege ya Nato dhidi ya mji wa Majr."
Jumuia ya kujihami ya NATO imekiri madege yake yamehujumu majengo mawili ya shughuli za kilimo yanayotumiwa,inasema kwa masilahi ya kijeshi."Hatuna ushahidi bado kama raia wameuwawa."amesema msemaji wa jumuia ya NATO Roland Lavoie.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Afp
Mhariri:Abdul-Rahman