1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kurejesha utoaji wa misaada ya chakula Ethiopia

Sylvia Mwehozi
15 Novemba 2023

Marekani imetangaza kurejesha utoaji wa msaada wa chakula nchini Ethiopia, baada ya serikali kukubali kuruhusu misaada hiyo kufuatiliwa.

https://p.dw.com/p/4Yob8
Addis Ababa | Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipotembelea Ghala la Kituo cha Usafirishaji cha Umoja wa Mataifa, mjini Addis Ababa.Picha: Tiksa Negeri/REUTERS

Marekani imetangaza kurejesha utoaji wa msaada wa chakula nchini Ethiopia, baada ya serikali kukubali kuruhusu misaada hiyo kufuatiliwa. Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani USAID, limetangaza kuanza upya utoaji wa chakula mwezi ujao kwa muda wa mwaka mmoja kwanza ili kuthibitisha kama serikali inatimiza ahadi zake.

Shirika hilo lilisitisha utoaji wa misaada yote ya chakula nchini Ethiopiamnamo mwezi Juni, baada ya kuwepo na ripoti za hujuma iliyoratibiwa ya kubadilisha njia ya usambazaji wa msaada wa chakula ili usiwafikie wenye mahitaji.

Marekani haikuwataja hadharani wahusika lakini mashirika ya misaada yalizilaumu pande zote, za mamlaka ya shirikisho na ya kikanda, huku wanajeshi wakinufaika kutokana na mauzo ya vyakula vilivyotolewa. Marekani imeikosoa vikali Ethiopia, dhidi ya kampeni yake ya kijeshi ya miaka miwili katika mkoa wa Tigray.