1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatakiwa kusitisha shughuli za kijeshi nchini Chad

20 Aprili 2024

Jeshi la anga la Chad limeiamuru Marekani kusitisha shughuli zake katika kituo cha anga cha Adji Kossei karibu na mji mkuu wa N'Djamena.

https://p.dw.com/p/4f014
Sahel | Wanajeshi wa Ufaransa wakiwa katika doria
Wanajeshi wa Ufaransa wakiwa katika eneo la Sahel katika oparesheni ya kukabiliana na makundi ya itikadi kali.Picha: Sebastien Rieussec/Hans Lucas/IMAGO

Katika barua iliowasilishwa kwa Waziri wa ulinzi wa Chad, mkuu wa jeshi la anga katika taifa hilo  Idriss Amine Ahmed amesema amemtaka mwambata wa kijeshi wa Marekanikusitisha shughuli kwenye kituo hicho cha wanaanga kwa sababu imeshindwa kutoa nyaraka za kuhalalisha uwepo wao.

Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani amesema mataifa hayo mawili yapo katika mazungumzo, kuhusu mustakabali wa ushirikiano wao katika masuala ya usalama.

Soma pia:Chad iko katika hali ya tahadhari baada ya shambulizi kwenye idara ya usalama

Marekani inao wanajeshi wapatao 100 nchini Chad, ambao wanahudumu kwa kupokezana zamu. Mkoloni wa zamani wa Chad, Ufaransa, inao wanajeshi 1000 na ndege za kivita katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati. 

Hadi sasa Chad haijachukua hatua kama mataifa mengine yanayotawaliwa kijeshi ya Burkina Faso, Mali na Niger katika kusitisha ushirikiano wa kijeshi na Ufaransa na mataifa mengine ya Magharibi.