1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasitisha misaada Somalia kufuatia madai ya wizi

8 Januari 2026

Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani wamewakemea vikali viongozi wa Somalia kufuatia madai ya wizi wa msaada wa chakula na kusitisha programu zote zinazoendelea za msaada wa Marekani kwa serikali ya Somalia.

https://p.dw.com/p/56Ut6
WFP I Mpango wa Chakula Duniani
Somalia inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za kiusalama na kiuchumi, huku Umoja wa Mataifa ikiiorodhesha miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani.Picha: Abukar Albadri/dpa/picture-alliance

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano, Marekani imesema imepokea ripoti kuwa maafisa wa Somalia waliharibu ghala la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, lililofadhiliwa na Marekani na kuchukua kinyume cha sheria tani 76 za chakula kilichokusudiwa kwa wananchi walio hatarini.

Marekani imesisitiza kuwa ina sera ya kutovumilia kabisa wizi au upotevu wa misaada na kwamba msaada wowote wa baadaye utategemea uwajibikaji wa serikali ya Somalia. Hata hivyo maafisa wa Somalia hawajatoa jibu rasmi kuhusu hatua ya Marekani.

Somalia, iliyopo katika Pembe ya Afrika, inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za kiusalama na kiuchumi, huku Umoja wa Mataifa ikiiorodhesha miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani.