1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaonya dhidi ya ruzuku ya China kwa viwanda

5 Aprili 2024

Waziri wa Fedha wa Marekani, Janet Yellen, ameonya kwamba ruzuku zinazotolewa na serikali ya China kwa viwanda vyake zinaweza kuvuruga ustahimilivu wa kiuchumi duniani.

https://p.dw.com/p/4eSSD
China | Janet Yellen na He Lifeng
Waziri wa Fedha wa Marekani, He Lifeng (kushoto) akiwa na Naibu Waziri Mkuu wa China, He Lifeng, wakati wa ziara yake mjini Beijing siku ya Ijumaa (Aprili 5).Picha: Andy Wong/AP/Pool/dpa/picture alliance

Katika ziara yake nchini China, Yellen ameelezea wasiwasi wake kuhusu uzalishaji wa kupita kiasi unaofanywa na makampuni ya China hasa kwenye uundaji wa vyombo na vifaa vya kielektroniki vinavyolielemea soko la dunia.

Akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Amerika mjini Guangzhou siku ya Ijumaa (Aprili 5), Yellen alisema angelijadiliana na China kuhusu "changamoto" zinazokabili biashara za Marekani nchini China.

Soma zaidi: Waziri wa Fedha wa Marekani kujadiliana ´mazito´ na China

"Uwezo wa kupita kiasi sio tatizo jipya, lakini umeimarishwa na tunaona hatari zinazojitokeza katika sekta mpya. Msaada wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja unaotolewa na serikali kwa sasa unaongeza uwezo wa uzalishaji ambao unapitiliza kwa kiwango kikubwa mahitaji ya ndani ya China." Alisema Yellen.

Waziri huyo wa fedha wa Marekani amekutana na Naibu Waziri Mkuu wa China, He Lifeng, ambaye alisema alitarajia mijadala ya kina zaidi kuhusu masuala muhimu ya kiuchumi na kifedha kwa China na Marekani.