Marekani yaamini suluhu itapatikana kabla ya kumalizika mwaka mashariki ya kati | Habari za Ulimwengu | DW | 04.05.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Marekani yaamini suluhu itapatikana kabla ya kumalizika mwaka mashariki ya kati

-

RAMALLAH

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice amelitaka taifa la Israel kufungua vizuizi vya usafiri dhidi ya wapalestina. Akizungumza mjini Ramallah leo hii na rais Mahmoud Abbas wa Palestina amewataka kwa upande mwingine wapalestina kuchukua hatua kuzuia mashambulio ya wanamgambo dhidi ya Israel. Aidha akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari amesema suluhisho la amani kati ya pande hizo mbili linaweza kupatikana kabla ya kumalizika mwaka huu. Awali Condolezza Rice ambaye yuko mashariki ya kati katika ziara ya kutia msukumo mazungumzo ya kutafuta amani kati ya waisrael na wapalestina alisema hatua ya Israel ya kujenga makazi ya walowezi wa kiyahudi katika ukingo wa magharibi ni tatizo na kikwazo kikubwa kuelekea amani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com