Marekani Olimpik yawaendea kombo | Michezo | DW | 22.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Marekani Olimpik yawaendea kombo

Wamarekani jana watupa chini vijiti katika mbio za kupokezana.

Katika mashindano ya riadha ya olimpik mjini Beijing,Veronica Campbell-Brown alikamilisha jana ushindi wa wajamaica wa kukumba medali zote za dhahabu upande wa wanaume na wanawake katika masafa ya mita 100 na 200.

kiroja cha mambo jana,wanariadha wa Marekani waliangusha vijiti vyao katika mbio za kupokezana tangu wanaume hata wanawake na sasa hawana matumaini ya medali.Marekani lakini, ilishinda jana mbio za mita 400 wanaume ilipotoroka na medali zote 2 -dhahabu na fedha.Timu ya wasichana wa Ujerumani-mabingwa wa dunia ilinyakua jana medali ya shaba wakati ile ya Brazil, iliondokea fedha.Mabingwa wa olimpik wa dimba, ni Marekani.

►◄

Ingawa mashindano ya masafa mafupi ya michezo ya olimpik ya Beijing kwa sehemu kubwa yamewaendea kombo wamarekani tangu upande wa wanaume hata wa wanawake, na Jamaica imeibuka dola kuu la mbio fupi za kasi, Marekani ilifuta jana machozi ilipotwaa taji la mita 400.LaShawn Merrit alimaliza enzi ya Muamerika mwenzake Jeremy Wariner alipompita na kunyakua medali ya dhahabu akimuachia ya fedha.

Marekani jana iliangusha vijiti vyake katika mbio za kupokezana tena zote 2-wanaume na wanawake na hii imewasangaza wengi kwavile, daima ni mbio zao :Kwanza ilikua Davis Patton na bingwa wa dunia Tyson Gay walitupa kijiti chao chini,halafu timu yao ya wasichana ikawaigiza pale Torri Edwards alimpotaka kumkabidhi Lauryn Williams.

Mbio za mita 110 kuruka viunzi ambazo China ilitazamia kutwaa medali yake ya dhahabu katika riadha, lilikwenda kwa bingwa wa rekodi ya dunia Dayron Robles.

Barbora Spotakova wa Jamhuri ya Czech akatoroka na medali ya dhahabu ya mchezo wa kurusha mkuki-javelin,lakini Russia ilinyakua medali ya dhahabu ilioletwa na Olga Kaniskina katika kutembea km 20 wanawake.

Medali ya dhahabu katika kuruka mara 3 wanaume-triple jump ilienda kwa Nelson Evora wa Ureno .

Ujerumani,Uingereza na Hungary ndizo zilizonyakua medali za kwanza za dhahabu asubuhi ya leo katika mashindano ya kupioga-makasia huko Beijing.timu ya wapigamakasia 4 ya ujerumani ya akina Fanny fischer,nicole reinhard,Katrin Wagner-Augustin na Conny Wasmuth walinyakua ushindi wa mbio za mita 500.

Mabingwa wapya wa dimba la olimpik upande wa wanawake ni Marekani na kwa mara nyengine tena Brazil imeshindwa kutawazwa mabingwa wa olimpik wa dimba tangu upande wa wanaume walipotolewa majuzi na argentina na jana na marekani katika finali.

Wameondokea na medali ya fedha upande wa wasichana.

Medali ya shaba ilienda jana kwa Ujerumani.

Je, mabingwa wa dunia waliridhika na medali hiyo ?

Alao stadi wao mmoja anasema ndio:

"Tulicheza kwa nguvu zaidi katika kipindi cha pili na mwishoe tulishinda medali ya shaba na yafaa kuridhika.Ingawa akatika kushambulia usoni nikitarajia mcheza bora zaidi."

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com