1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuunga mkono amani ya mashariki ya kati

Siiraj Kalyango29 Novemba 2007

Marekani pia imeonya kuwa juhudi hizi mpya za kuwapatanisha waIsrael na wa Palestina zikishindwa ,umwagikaji zaidi wa damu unaweza ukatokea.Hata hivyo kunashakashaka ikiwa kweli mapatano yataweza kufikiwa hapo mwakani.

https://p.dw.com/p/CUiT
Abbas,kulia Bush katikati, na Olmert wakiwa Marekani.Picha: AP

Ahadi ya serikali ya Marekani, imetolewa na rais wake George W. Bush,baada ya kukutana na viongozi wa Israel na Palestina katika Ikulu ya White- House kufuatia pande mbili hasimu kuahidi kufikia mapatano ya amani mwishoni mwa mwaka ujao wa 2008.

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza,Tony Blair,asema umuhimu wa mkutano ambao umekuja kujulikana kama mkutano wa Annapolis.

O-TON 1-BLAIR…

‘jambo muhimu hasa katika mkutano wa Annapolis ni kuwa umezindua harakati na ratiba maalum nfano mwaka 2008,na sio kuzungumzia baadhi ya masuala lakini kutanzua masuala yote muhimu kati ya Israel na palestina.’

Yeye msemaji wa waziri mkuu wa Israel,Miri Eisin nae amegusia umuhimu wa mkutano huo kutokana na viongozi wa Palestina na Israel kuhudhuria wenyewe mazungmzo hayo.

O-TON MIRI EISIN…

Kutokana na kuwa wamekuja mwanzo wa majadiliano,na baadae wakaaumua kuzungumzia kuhusu jinsi watakavyoshirikishwa na wala sio kupatanisha.

Wapalestina na Waisrael wamekaa chini pamoja ana kwa ana. Na ndio wao wana hitaji kusukuma mbele majadiliano.Wapo , wanajihusisha na hawako kando wakingoja kuona kile kitakachofuata.

Hata hivyo matatizo yanayozikabili pande mbili,yamedhihirishwa na hujuma mpya za Israel dhidi ya Hamas katika ukanda wa Gaza.

Ndege za kijeshi za Israel zimefanya hujuma katika ukanda huo.Wanaharakati wanne wa Hamas waliuliwa. Kundi la Hamas linasisitiza kuwa Wapalestina hawataheshimu maamuzi yoyote yatakayofikiwa katika mkutano wa amani ya mashariki ya kati ,unaofanyika Marekani wiki hii.

Kundi la kijeshi la Hamas, Ezzedine Al-qassim Brigades, limetoa taarifa likisema kuwa njia zote zipo za kujibu makosa,hususan baada ya mkutano wa Annapolis ambayo yametoa ruksa kutenda unyama zaidi dhidi ya wananchi.

Aidha Hamas limeonya uongozi wa Palestina dhidi ya ahadi zao za kutekeleza ratiba ya amani ya mashariki ya kati,kama ilivyokuwa katika tamko la pamoja baada ya pande mbili kusema kuwa zimekubaliana kabla ya kuanza mkutano wa Marekani siku ya jumanne.