1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani haina mkakati Iraq ?

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTQ

LONDON:

Jamadari mwengine wa hadhi ya juu wa Uingereza,amekosoa hadharani tena wazi wazi mkakati wa Marekani nchini Iraq.

Katika mahojiano kwenye toleo la leo la gazeti la Uingereza la SUNDAY MIRROR,Meja-jamadari Tim Cross ameieleza sera ya marekani nchini Irak ilokwenda kombo vibaya sana.“

Akaliambia gazeti hilo kwamba alikwishaelezea wasi wasi wake waziri wa zamani wa ulinzi wa marekani Donald Rumsfeld juu ya kutokuwapo mpango maalumu uliofuatia vita,lakini Bw. Rumpsfeld alidharau maonyo yote.

Ila za Meja-jenerali Cross zimeibuka baada ya mkuu wa zamani wa jeshi la Uingereza,jamadari Mike Jackson,kueleza mkakati wa Marekani nchini Irak kuwa „ uliofilisika kiakili“.