Maoni ya wahariri | Magazetini | DW | 09.02.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri

Hatima ya chama cha FDP na siri za mabenki.

Guido Westerwelle na Kansela Merkel.

Guido Westerwelle na Kansela Merkel.

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani, leo yametuwama mno juu ya mada za ndani:Usoni kabisa, ni hali inayojikuta chama cha kiliberali cha Free Democratic Paerty (FDP) katika serikali ya muungano ya Ujerumani chini ya uongozi wa Kanzela Angela Merkel. Maoni yameonesha kuwa ,FDP imeanza vibaya serikalini.Pia mkasa wa siri za mabenki ya Uswisi kwa akiba za watoro wa kodi, ungali unagonga vichwa vya habari lakini pia, uchaguzi wa urais nchini Ukraine.

Gazeti la DRESDNER NEUSTE NACHRICHTEN juu ya matokeo ya uchaguzi wa Ukraine laandika:

Je, Janukowitsch ni mtu barabara aliechaguliwa ? lauliza gazeti.Laendelea kuandika kwamba, rais huyu mpya ana doa la kupitisha mizengwe katika uchaguzi na kwamba, ni mwanasiasa alie karibu na Moscow.Lakini, hata madoa hayo, hayakumzuia asichaguliwe rais na wapiga kura .Yadhihirika kwa hivyo, watawala wa hadi sasa, walishindwa kabisa.Nchi kama Ukraine,yaweza tu kujizatiti kwa kuweka wezani kati ya maslahi ya kambi ya magharibi na mashariki ; na Janukowitsch,haoneshi ndie mtu anaefaa kwa hayo.

Likitugeuzia mada na kuturejesha katika ule mkasa wa siri za mabenki , waziri wa fedha wa Ujerumani Bw.Wolfgang Schäuble,anahisi:

Mtindo wa kuweka siri akiba za fedha za wateja wake Uswisi, hauna mustakbala mwema wakati huu.Mtindo huo umeshafikia mwisho wake.

Wakati huu Bunge la Ulaya na Kamisheni ya Ulaya zinavutana katika kuitikia au la, ombi la Marekani la kutaka kutumia taarifa za nyendo za fedha za wakaazi wa Umoja wa Ulaya, maarufu (SWIFT) .Kwanini basi ,kuna mvutano huo ikiwa desturi ya kuweka siri za kibenki sasa inakoma na inaweza siri hiyo kuingiliwa na mkono wa serikali ?-lauliza gazeti .Kulinda taarifa za banki, ni kwa masilahi ya kila mmoja, lasema Berliner Zeitung.

Likigeukia hali inayojikuta chama cha kiliberali cha FDP serikalini wakati huu, gazeti la Nüremberger Nachrichten laandika:

"Katika uchunguzi wa maoni ya wananchi , chama cha FDP miezi 3 na nusu tangu ushindi wake mkuu katika uchaguzi uliopita ,kimerejea katika kipimo chake cha kawaida cha umaarufu.Hali hiyo ingawa inawafurahisha raia wengi waliovunjika moyo, lakini haitathiri kitu kama mshindo wa viongozi wake waliotoa baada ya kikao cha dharura cha Jumapili ulivyoonesha.

Kile wanachohitaji viongozi wake akina Bw.Westerwelle,Lindner,Rösler na wenzao ni pigo kali ili waamke kutoka ulimwengu wa ndoto zao za uliberali.Nafasi ya kuwazindua kutoka usingizi huo itakuja Mei 9 pale ingawa kwa bahati mbaya, ni katika mkoa mmoja tu wa Northrhein-Westfalia utapofanyika uchaguzi .

Likiendelea na mada hii, gazeti la MINDENER TAGBLATT laandika kwamba, bila ya shaka FDP , kimetafsiri vibaya matokeo ya uchaguzi uliopita wa Bunge la Shirikisho kwa kutaka kuonesha shukurani tu kwa wale wapigakura waliokipa ushindi ule na ambao wangependa kuigeuza nchi hii mpaka katika jiwe lake la msingi iwe ya kiliberali. Gazeti laongeza:

"Kuna wengine waliotaka mageuzi tu ya serikali ..............Sasa kuwabebesha hawa mzigo wa mageuzi kama hayo,kunakumbana na pingamizi zao."

Mwandishi: Ramadhan Ali/ DPA

Uhariri: Abdul-Rahman